Skip to main content
Guidance

Kurudi Kenya (accessible)

Published 15 September 2026

Ni msaada mgani unoatolewa?

Taarifa kabla ya kuondoka

  • Watu wanaorejea wanaweza kuwasiliana na IRARA kujadili chaguzi za kujumuika tena nchini Kenya.

Msaada wa muda mfupi

  • Mapokezi katika uwanja wa ndege (ikiwa imeombwa)
  • Malazi kwa hadi usiku 5
  • Usafiri kwenda kwenye kituo ndani ya nchi
  • Usaidizi wa chakula na mahitaji ya kimsingi
  • Msaada mdogo wa fedha kwa mahitaji ya dharura

Kumbuka: Huduma hizi zinapatikana tu ndani ya siku 5 baada ya kuwasili Kenya.

Msaada wa muda wa kati

  • Msaada wa kutafuta na kuunganishwa tena na familia
  • Msaada wa kupata vitambulisho nchini
  • Uelekezaji kwa huduma za ndani (referrals)
  • Msaada wa afya ya akili

Msaada wa muda mrefu

Usaidizi wa Kielimu na Ujasiriamali kwa warejeaji.

  • Msaada wa kupata ajira katika soko la ndani
  • Msaada wa kuanzisha biashara
  • Msaada wa kupata mafunzo ya ufundi au elimu ya juu
  • Msaada wa fursa za uhamiaji wa kisheria kwenda nchi ya tatu

Nani anaweza kupata msaada?

Ikiwa wewe ni raia wa Kenya ambaye amerudi au atarejeshwa kutoka Uingereza, IRARA inaweza kukusaidia kujenga upya maisha yako nchini Kenya.

Ikiwa unahitaji msaada, lazima uwasiliane na IRARA ndani ya miezi 3 baada ya kurudi kwako. Msaada utapatikana kwa muda wa hadi miezi 12.

Jinsi ya kupata msaada?

Ikiwa uko kwa sasa nchini Uingereza, wasiliana na ofisi ya IRARA ya UK kwa kutumia maelezo yaliyo hapa chini. Ikiwa tayari umerudi Kenya, tafadhali wasiliana na ofisi ya IRARA iliyoko Nairobi kwa kutumia maelezo yaliyo hapa chini.

Kuhusu Mradi

Mpango wa Kurudi na Kujumuishwa Tena wa UK Home Office unasaidia watu walioko Uingereza ambao hawana hadhi ya kisheria au ruhusa ya kubaki nchini humo.

Mpango huu unatoa huduma mbalimbali, ikiwa ni pamoja na msaada wa mapokezi na msaada wa muda mrefu kwa watu wanaorudi Kenya.

Kuhusu IRARA

IRARA imekuwa ikisaidia watu binafsi na familia kwa miaka mingi kuweza kujumuika tena katika jamii ya Kenya na kujenga upya maisha yao.

Washauri wao wenye uzoefu hufanya kazi kote nchini kutoa msaada wa kitaalamu na uliobinafsishwa kwa watu wanaostahiki wanaorejea kutoka Ireland, ili kuhakikisha mchakato wa kurudi unakuwa rahisi na endelevu.

Maelezo ya mawasiliano nchini Kenya

IRARA Kenya,
Jengo la The Address
Ghorofa ya 7
Muthangari Drive
Parklands,S.L.P
PO Box 650-0060
Nairobi

Saa za kazi: Jumatatu – Ijumaa, saa 3 asubuhi – saa 11 jioni

Barua pepe: reintegration@irara.org

Simu: + 254 707 251948

Saa za kazi za IRARA UK

Saa 2:30 asubuhi – saa 11 jioni, Jumatatu – Ijumaa

Simu: +44 (0)1433 627 247

Barua pepe: reintegration@irara.org